Sherehekea mwaka wa 2025 ukitumia Marudio ya Picha kwenye Google 🎉 Pata yako sasa kwenye programu

Skip to main content

Cheza tena matukio ya 2025 ukitumia Recap

Ni wakati wa kusherehekea mwaka wako! Marudio ya Picha kwenye Google ni mkusanyiko wa picha za watu unaowapenda, matukio ambayo hayajapangwa na mengineyo. Jikumbushe matukio yako bora sasa. 1

Nufaika zaidi na kila kumbukumbu

GB 15 za nafasi ya hifadhi2

Hiyo ni mara 3 zaidi ya huduma nyingine nyingi za hifadhi ya wingu.

Cloud icon with a checkbox

Unapata GB 15 za nafasi ya hifadhi, ili uweze kuhifadhi nakala na kuweka kumbukumbu zako salama kiotomatiki — bila malipo.2

Zana zinazotumia AI

Hariri, panga, tafuta na zaidi.

Wand icon with sparkles

Boresha picha zako, pata kwa urahisi picha unazotafuta na uzipange kiotomatiki - yote haya ukitumia uwezo wa AI kutoka Google.

Je, unatumia iPhone®?3 Tumekushughulikia.

Programu ya Picha kwenye Google inakufaa. Unaweza kusawazisha maktaba na maudhui unayopenda wakati wa kuweka mipangilio na picha zako zitapakiwa kiotomatiki kwenye programu.

Wand with sparkles

Picha zilizoboreshwa kwa kutumia Google AI

Kihariri Mahiri.

Hariri picha kwa kina kwa kugusa mara chache tu.

Kifutio cha Ajabu.

Vipengele vinavyovuruga ni kumbukumbu ya zamani.

Kifuta Ukungu.

Badilisha picha zenye ukungu ziwe za kuvutia.

Jikumbushe matukio ya zamani

Angalia tena kumbukumbu unazopenda kwa urahisi. Kupitia mfumo wa mashine kujifunza, picha zako bora zinaratibiwa ili uweze kuzituma kwa watu waliofanya matukio hayo yawe ya kipekee.

Yamepangwa kwa usaidizi wa AI

Picha na hati zako hupangwa kiotomatiki, ili uweze kutumia muda mwingi kufurahia kumbukumbu zako na muda mchache kuzipanga.

Photo Stacks feature indicating 3 photos are stacked. Photo Stacks feature indicating 3 photos are stacked. Photo Stacks feature indicating 3 photos are stacked.

Panga picha zinazofanana kiotomatiki ukitumia kipengele cha Picha Zinazofanana

Documents tab showing the number of each type of document within the app. Documents tab showing the number of each type of document within the app. Documents tab showing the number of each type of document within the app.

Hati hupangwa katika albamu, kama vile picha za skrini, stakabadhi za malipo, madokezo na zaidi.

A couple smiling and hugging for a selfie.

Waonyeshe wengine tabasamu

Tumia mtu yeyote katika anwani zako picha, video na albamu kwa urahisi — hata kama hatumii huduma ya Picha kwenye Google.

Message, photo and copy link icons.

Tuma kwenye programu za kila siku

Tuma albamu au picha kwa marafiki kwenye programu unazopenda kutumia kila siku kama vile WhatsApp, Snapchat na nyinginezo.

Icons indicating trusted users within the Google Photos app.

Tuma kwa
mtu unayemwamini

Tuma kiotomatiki picha za watu na wanyama vipenzi uliochagua kwa mshirika au mtu unayemwamini zaidi.

Eneo salama la kuweka kumbukumbu za maisha

Data yako ni yako

Kila kitu unachoweka kwenye Picha kwenye Google ni chako na unaweza kufuta au kuhamisha maudhui yako wakati wowote.

Padlock icon indicating security.

Kumbukumbu zako ziko salama

Tunaendesha mojawapo ya mifumo bora zaidi ya usalama ili kusaidia kulinda usalama wa picha na video zako.

A checkmark icon.

Data yako haitumiki kwenye matangazo

Programu ya Picha kwenye Google haiuzi kamwe picha, video au taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote na hatutumii picha na video zako kwa matangazo.

Maswali yanayoulizwa sana

Kila Akaunti ya Google huwa na GB 15 za nafasi ya hifadhi ya kutumia kwenye huduma ya Picha kwenye Google, Gmail na Hifadhi ya Google. Unaweza pia kununua nafasi zaidi ya hifadhi ukitumia mpango wa uanachama wa Google One.

Ndiyo, Picha kwenye Google hufanya kazi kwenye vifaa vya iOS na Android. Pakua programu ili uanze. Unaweza pia kuitumia kwenye vifaa vya Kompyuta na Vishikwambi. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi programu ya Picha kwenye Google inavyojumuishwa na matunzio chaguo msingi ya kifaa chako.

Unaweza kuhifadhi picha na video zako kiotomatiki kwenye Akaunti yako ya Google unapowasha kipengele cha kuhifadhi nakala. Unaweza kuwasha kipengele cha kuhifadhi nakala unapoweka mipangilio ya programu yako ya Picha au ukienda kwenye ukurasa wa Mipangilio na uwashe kipengele cha kuhifadhi nakala. Unaweza pia kuhifadhi nakala za picha zako mwenyewe. Pata maelezo zaidi kuhusu manufaa ya kuhifadhi nakala.

Ili kuhariri picha kwenye kifaa chako cha mkononi, pakua na usakinishe programu ya Picha kwenye Google. Vipengele vya kuhariri ikiwa ni pamoja na Kifutio cha Ajabu na Kifuta Ukungu vinapatikana tu kwenye programu ya Picha kwenye Google. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuhariri picha na video zako.

Unaweza kutuma picha, video, albamu na video za matukio muhimu kwa mtu yeyote katika anwani zako, hata kama hatumii programu ya Picha kwenye Google. Gusa tu kitufe cha “Tuma” na utaweza kutuma picha moja kwa moja kwa watumiaji waliopo wa programu ya Picha kwenye Google au uguse “Tuma kwa” ili utume kwa anwani zako, utume kwenye programu unazotumia kila siku, uunde albamu ya pamoja au uunde kiungo cha moja kwa moja cha picha hiyo. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutuma picha na video zako.

Unaweza kutafuta chochote kwenye picha na video zako kwa urahisi. Kwa mfano, unaweza kutafuta kulingana na maeneo uliyotembelea, mnyama wako kipenzi, vyakula unavyopenda na zaidi. Ili utafute na udhibiti picha zako kwa urahisi, unaweza kuwapa watu au wanyama vipenzi wanaoonekana jina kwenye picha zako. Pata maelezo zaidi kuhusu Nyuso Zinazofanana na jinsi ya kutafuta picha zako.

Pakua programu ya Picha kwenye Google

Hifadhi nakala ya kumbukumbu za picha zako kwenye vifaa vyako vyote.

Changanua ili upate programu ya Picha